Skip to content

Matamshi ya Shurti katika Nuru

Matamshi ya shurti katika Nuru yanatumika kutekeleza utendaji tofauti kulingana na masharti fulani. Tamshi la kama/sivyo muundo wa msingi kudhibiti ambao unakuwezesha kutekeleza msimbo kwa kulingana na masharti maalum. Ukurasa huu unaangazia misingi ya tamshi la kama/sivyo katika Nuru.

Kama

Tamshi la kama linaanza na neno msingi kama, likifuatiwa na mabano ya sharti. Kama sharti ni kweli, msimbo ndani ya mabano singasinga utatekelezwa.

go
kama (2 > 1) {
    andika(kweli) // Tokeo: kweli
}
kama (2 > 1) {
    andika(kweli) // Tokeo: kweli
}

Katika huu mfano, sharti 2 > 1 ni kweli, hivyo tamshi la andika(kweli) litatekelezwa na tokeo litakua kweli.

Au Kama na Sivyo

Unaweza kutumia au kama kujaribisha masharti mengi na sivyo kubainisha pande la msimbo litakalotekelezwa pale ambapo masharti yote sio kweli.

go

fanya a = 10

kama (a > 100) {
    andika("a imezidi 100")
} au kama (a < 10) {
    andika("a ndogo kuliko 10")
} sivyo {
    andika("Thamani ya a ni", a)
}

// Tokeo litakua: 'Thamani ya a ni 10'

fanya a = 10

kama (a > 100) {
    andika("a imezidi 100")
} au kama (a < 10) {
    andika("a ndogo kuliko 10")
} sivyo {
    andika("Thamani ya a ni", a)
}

// Tokeo litakua: 'Thamani ya a ni 10'

Katika huu mfano, sharti la kwanza a > 100 sikweli, na kwenye sharti la pili a < 10 pia sikweli. Hivyo basi, msimbo ndani ya pande la sivyo unatekelezwa, na tokeo ni "Thamani ya a ni 10".

Kwa kutumia matamshi ya kama/sivyo ikiwa na maneno msingi kama, au kama, na sivyo, utaweza kudhibiti mtiririko wa msimbo wako wa Nuru kwa kuzingatia masharti tofauti.

All code is open source if you can read Assembly