Tupu in Nuru
Katika Nuru, aina ya data tupu huwakilisha kutokuwepo kwa thamani au dhana ya "hakuna kitu". Ukurasa huu unaangazia sintaksia na matumizi ya aina ya data tupu katika Nuru, ikiwemo ainisho na tathmini.
Ainisho
Aina ya data tupu ni aina ya data ambayo haina kitu, ikiainishwa na neno msingi tupu
:
go
fanya a = tupu
fanya a = tupu
Tathmini
Wakati wa kutathmini data ambayo ni tupu kwenye semi za masharti, thathmini yake itakua sikweli:
go
kama (a) {
andika("nimevaa nguo")
} sivyo {
andika("nipo tupu")
}
// Output: nipo tupu
kama (a) {
andika("nimevaa nguo")
} sivyo {
andika("nipo tupu")
}
// Output: nipo tupu
Aina ya data tupu inamanufaa wakati unapohitaji kuwakilisha thamani ambayo haijaanzishwa, inakosekana, au haijaainishwa katika programu zako. Kwa kuelewa aina ya data tupu
, utaweza kutengeneza msimbo ambao ni imara na nyambufu.