Safu Katika Nuru
Safu katika nuru ni miundo ya data ambayo inaweza kubeba vitu vingi, ikiwa ni pamoja na aina za data tofauti tofauti kama namba
, tungo
, buliani
, vitendakazi
, na thamani tupu
. Ukurasa huu unaangazia vipengele mbalimbali vya safu, ikiwemo namna ya kutengeneza, kuchambua, na kuzunguka ndani yake kwa kutumia vitendakazi vilivyojengwa ndani ya Nuru.
Kutengeneza Safu
Kutengeneza safu, tumia mabano mraba na tenganisha kila kitu kimoja kwa kutumia mkwaju:
orodha = [1, "pili", kweli]
orodha = [1, "pili", kweli]
Kupata na Kubadilisha Vipengele vya Safu
Safu katika Nuru ni zero-indexed; ikimaanisha kipengele cha kwanza katika safu kina kumbukumbu namba 0. Kupata kipengele, unaweza ukatumia kumbukumbu namba yake ndani ya mabano mraba:
namba = [10, 20, 30]
jina = namba[1] // jina is 20
namba = [10, 20, 30]
jina = namba[1] // jina is 20
Unaweza ukabadilisha kipengele katika safu kwa kutumia kumbukumbu namba yake:
namba = [10, 20, 30]
namba[1] = 25
andika(namba) // Tokeo: [10,25,30]
namba = [10, 20, 30]
namba[1] = 25
andika(namba) // Tokeo: [10,25,30]
Kuunganisha Safu
Kuunganisha safu mbili au zaidi, tumia kiendeshi +
:
a = [1, 2, 3]
b = [4, 5, 6]
c = a + b
// c is now [1, 2, 3, 4, 5, 6]
a = [1, 2, 3]
b = [4, 5, 6]
c = a + b
// c is now [1, 2, 3, 4, 5, 6]
Kuangalia Uanachama Katika Safu
Tumia neno msingi ktk
kuangalia kama kipengele kipo ndani ya safu:
namba = [10, 20, 30]
andika(20 ktk namba) // Tokeo: kweli
namba = [10, 20, 30]
andika(20 ktk namba) // Tokeo: kweli
Kuzunguka Ndani ya Safu
Unaweza kutumia maneno msingi kwa
na ktk
kuzunguka ndani ya safu. Kuzunguka ndani ya safu na kupata kipengele peke yake tumia sintaksia ifuatayo:
namba = [1, 2, 3, 4, 5]
kwa thamani ktk namba {
andika(thamani)
}
//Tokeo:
1
2
3
4
5
namba = [1, 2, 3, 4, 5]
kwa thamani ktk namba {
andika(thamani)
}
//Tokeo:
1
2
3
4
5
Kuzunguka ndani ya safu na kupata kumbukumbu namba na kipengele tumia sintaksi aifuatayo:
majina = ["Juma", "Asha", "Haruna"]
kwa idx, jina ktk majina {
andika(idx, "-", jina)
}
//Tokeo:
0-Juma
1-Asha
2-Haruna
majina = ["Juma", "Asha", "Haruna"]
kwa idx, jina ktk majina {
andika(idx, "-", jina)
}
//Tokeo:
0-Juma
1-Asha
2-Haruna
Vitendakazi vya Safu
Nuru ina vitendakazi mbalimbali vilivyojengwa ndani kwa ajili ya Safu:
idadi()
idadi()
hurudisha urefu wa safu:
a = [1, 2, 3]
urefu = a.idadi()
andika(urefu) // Tokeo: 3
a = [1, 2, 3]
urefu = a.idadi()
andika(urefu) // Tokeo: 3
sukuma()
sukuma()
huongeza kipengele kimoja au zaidi mwishoni mwa safu:
a = [1, 2, 3]
a.sukuma("s", "g")
andika(a) // Tokeo [1, 2, 3, "s", "g"]
a = [1, 2, 3]
a.sukuma("s", "g")
andika(a) // Tokeo [1, 2, 3, "s", "g"]
yamwisho()
yamwisho()
hurudisha kipengele cha mwisho katika safu, au tupu
kama safu haina kitu:
a = [1, 2, 3]
mwisho = a.yamwisho()
andika(mwisho) // Tokeo: 3
b = []
mwisho = b.yamwisho()
andika(mwisho) // Tokeo: tupu
a = [1, 2, 3]
mwisho = a.yamwisho()
andika(mwisho) // Tokeo: 3
b = []
mwisho = b.yamwisho()
andika(mwisho) // Tokeo: tupu
Kwa kutumia taarifa hii, unaweza ukafanyakazi na safu za Nuru kwa ufanisi, kufanya iwe rahisi kuchambua mikusanyo ya data katika programu zako.