Skip to content

Vitendakazi Vilivyojengwa Ndani ya Nuru

Nuru ina vitendakazi kadhaa vilivyojengwa ndani vinavyofanya kazi husika.

Kitendakazi andika()

Kitendakazi andika() kinatumika kuchapisha ujumbe kwenye konsoli. Inawezakuchukua hoja sifuri au zaidi, na hoja zitachapishwa na nafasi kati yao. Kwa kuongeza, andika() huhimili uundaji wa msingi kama vile /n kwa ajili ya mstari mpya, /t kwa ajili ya nafasi ya kichupo, na \\ kwa ajili ya mkwajunyuma. Mfano:

go
andika(1, 2, 3) // Output: 1 2 3
andika(1, 2, 3) // Output: 1 2 3
go
andika("Jina: Asha /n Umri: 20 /n Chuo: IFM")

// Output:
// Jina: Asha
// Umri: 20
// Chuo: IFM
andika("Jina: Asha /n Umri: 20 /n Chuo: IFM")

// Output:
// Jina: Asha
// Umri: 20
// Chuo: IFM

Kitendakazi jaza()

Kitendakazi jaza() kinatumika kupata ingizo kutoka kwa mtumiaji. Inawezakuchukua hoja sifuri au moja, ambayo ni utungo utakao tumika kama kimahasishi kwa mtumiaji. Mfano:

go
fanya salamu = unda() {
    fanya jina = jaza("Unaitwa nani? ")
    andika("Mambo vipi", jina)
}

salamu()
fanya salamu = unda() {
    fanya jina = jaza("Unaitwa nani? ")
    andika("Mambo vipi", jina)
}

salamu()

Katika mfano huu, tunaainisha kitendakazi salamu() ambacho kinamhamasisha mtumiaji kuingiza jina kwa kutumia kitendakazi jaza(). Kisha tunatumia kitendakazi andika() kuchapisha ujumbe unaobeba jina la mtumiaji aliloingiza.

Kitendakazi aina()

Kitendakazi aina() kinatumika kutambua aina ya kitu. Inakubali hoja moja, na thamani inayorudi hua ni utungo unaoonyesha aina ya kitu. Mfano:

go
aina(2) // Output: "NAMBA"
aina("Nuru") // Output: "NENO"
aina(2) // Output: "NAMBA"
aina("Nuru") // Output: "NENO"

Kitendakazi fungua()

Kitendakazi fungua() kinatumika kufungua faili. Inakubali hoja moja, ambayo ni njia ya faili unalotaka kufungua. Mfano:

go
faili = fungua("data.txt")
faili = fungua("data.txt")

Katika mfano huu, tumetumia kitendakazi fungua() kufungua faili linaloitwa "data.txt". Kibadilika faili kinabeba kumbukumbu ya faili lililofunguliwa.

All code is open source if you can read Assembly