Wakati Katika Nuru
Vitanzi vya wakati katika Nuru hutumika kutekeleza pande la msimbo kwa kujirudia maadam sharti lililopewa ni kweli. Ukurasa huu utaangazia Vitanzi vya wakati ikiwemo jinsi ya kutumia maneno msingi vunja
na endelea
ndani yake.
Sintaksia
Kitanzi cha wakati hutekelezwa pale ambapo sharti lililopo ni kweli. Unaanzisha kitanzi cha wakati kwa kutumia neno msingi wakati
likifwatiwa na sharti katika mabano ()
. Matokeo ya kitanzi yanatakiwa kuwekwa ndani ya mabano singasinga {}
:
fanya i = 1
wakati (i <= 5) {
andika(i)
i++
}
// Tokeo:
1
2
3
4
5
fanya i = 1
wakati (i <= 5) {
andika(i)
i++
}
// Tokeo:
1
2
3
4
5
Vunja and Endelea
Break (Vunja)
Tumia neno msingi vunja
kusitisha kitanzi:
fanya i = 1
wakati (i < 5) {
kama (i == 3) {
andika("nimevunja")
vunja
}
andika(i)
i++
}
// Tokeo:
1
2
nimevunja
fanya i = 1
wakati (i < 5) {
kama (i == 3) {
andika("nimevunja")
vunja
}
andika(i)
i++
}
// Tokeo:
1
2
nimevunja
Endelea
Tumia neno msingi endelea
kuruka mzunguko maalum:
fanya i = 0
wakati (i < 5) {
i++
kama (i == 3) {
andika("nimeruka")
endelea
}
andika(i)
}
// Tokeo:
1
2
nimeruka
4
5
fanya i = 0
wakati (i < 5) {
i++
kama (i == 3) {
andika("nimeruka")
endelea
}
andika(i)
}
// Tokeo:
1
2
nimeruka
4
5
Kwa kuelewa Vitanzi vya wakati katika Nuru, unaweza kutengeneza msimbo ambao unajirudia kufanya jambo fulani au kuangalia masharti fulani, na kukupatia unyumbulifu na udhibiti katika utekelezaji wa misimbo yako.