NAMBA KAMILI NA DESIMALI
Nambari kamili na desimali ni aina za msingi za data katika Nuru, zinazotumiwa kuwakilisha nambari nzima na nambari za desimali, mtawalia. Ukurasa huu unashughulikia sintaksia na matumizi ya nambari kamili na desimali katika Nuru, ikijumuisha utangulizi, nyongeza zisizo za kawaida, kazi za mkato, na nambari hasi.
UTANGULIZI
Nambari kamili na desimali hufanya kama inavyotarajiwa katika shughuli za hisabati, kwa kufuata kanuni ya MAGAZIJUTO:
2 + 3 * 5 // 17
fanya a = 2.5
fanya b = 3/5
a + b // 2.8
2 + 3 * 5 // 17
fanya a = 2.5
fanya b = 3/5
a + b // 2.8
ONGEZEKO ISIYO YA KAWAIDA
Unaweza kufanya nyongeza zisizo za kawaida (++ na --) kwa desimali na nambari kamili. Hizi zitaongeza au kupunguza 1 kutoka kwa thamani ya sasa. Kumbuka kuwa desimali au namba kamili lazima iwe imepewa kihifadhi ili operesheni hii ifanye kazi. Hapa kuna mfano:
fanya i = 2.4
i++ // 3.4
fanya i = 2.4
i++ // 3.4
KAZI ZA MKATO
Nuru inaauni kazi za mkato kwa +=, -=, /=, *=, na %=:
fanya i = 2
i *= 3 // 6
i /= 2 // 3
i += 100 // 103
i -= 10 // 93
i %= 90 // 3
fanya i = 2
i *= 3 // 6
i /= 2 // 3
i += 100 // 103
i -= 10 // 93
i %= 90 // 3
NAMBARI HASI
Nambari hasi pia hufanya kama inavyotarajiwa:
fanya i = -10
wakati (i < 0) {
andika(i)
i++
}
fanya i = -10
wakati (i < 0) {
andika(i)
i++
}
Pato:
-10
-9
-8
-7
-6
-5
-4
-3
-2
-1
0
1
2
3
4
5
6
7
8
9
-10
-9
-8
-7
-6
-5
-4
-3
-2
-1
0
1
2
3
4
5
6
7
8
9