Vitanzi Vya Kwa Katika Nuru
Vitanzi vya kwa ni muundo msingi wa udhibiti katika Nuru ambavyo hutumika kuzunguka vitu vinavyozungukika kama tungo, safu, na kamusi. Ukurasahuu unaangazia sintaksia na matumizi ya Vitanzi katika Nuru, ikiwemo kuzunguka ndani ya jozi ya funguo-thamani, na matumizi ya matamshi vunja na endelea.
Sintaksia
Kutengeneza kitanzi cha kwa, tumia neno msingi kwa likifwatiwa na kitambulishi cha muda mfupi kama vile i au v na kitu kinachozungukika. Funga mwili wa kitanzi na mabano singasinga {}. Mfano unaotumia tungo:
jina = "lugano"
kwa i ktk jina {
andika(i)
}
// Tokeo:
l
u
g
a
n
ojina = "lugano"
kwa i ktk jina {
andika(i)
}
// Tokeo:
l
u
g
a
n
oKuzunguka Ndani ya Jozi ya Funguo-Thamani
Kamusi
Nuru inakuruhusu kuzunguka ndani ya kamusi kupata thamani moja moja au jozi ya funguo na thamani yake. Kupata tu thamani, tumia kitambulisha cha muda mfupi:
kamusi = {"a": "andaa", "b": "baba"}
kwa v ktk kamusi {
andika(v)
}
// Tokeo:
andaa
babakamusi = {"a": "andaa", "b": "baba"}
kwa v ktk kamusi {
andika(v)
}
// Tokeo:
andaa
babaKupata thamani ya funguo na thamani zake, tumia vitambulishi vya muda mfupi viwili:
kwa k, v ktk kamusi {
andika(k + " ni " + v)
}
// Tokeo:
a ni andaa
b ni baba
kwa k, v ktk kamusi {
andika(k + " ni " + v)
}
// Tokeo:
a ni andaa
b ni babaTungo
Kuzunguka juu ya thamani za tungo, tumia kitambulishi cha muda mfupi:
kwa v ktk "mojo" {
andika(v)
}
// Tokeo:
m
o
j
okwa v ktk "mojo" {
andika(v)
}
// Tokeo:
m
o
j
oKuzunguka juu ya funguo na thamani zake, tumia vitambulishi vya muda mfupi viwili:
kwa i, v ktk "mojo" {
andika(i, "->", v)
}
// Tokeo:
0 -> m
1 -> o
2 -> j
3 -> okwa i, v ktk "mojo" {
andika(i, "->", v)
}
// Tokeo:
0 -> m
1 -> o
2 -> j
3 -> oSafu
Kuzunguka juu ya thamani za safu, tumia kitambulishi cha muda mfupi:
majina = ["juma", "asha", "haruna"]
kwa v ktk majina {
andika(v)
}
// Tokeo:
juma
asha
harunamajina = ["juma", "asha", "haruna"]
kwa v ktk majina {
andika(v)
}
// Tokeo:
juma
asha
harunaKuzunguka juu ya funguo na thamani katika safy, tumia vitambulishi vya muda mfupi viwili:
kwa i, v ktk majina {
andika(i, "-", v)
}
// Tokeo:
0 - juma
1 - asha
2 - harunakwa i, v ktk majina {
andika(i, "-", v)
}
// Tokeo:
0 - juma
1 - asha
2 - harunaVunja na Endelea
Vunja
Tumia neno msingi vunja kisitisha kitanzi:
kwa i, v ktk "mojo" {
kama (i == 2) {
andika("nimevunja")
vunja
}
andika(v)
}
// Tokeo:
m
o
j
nimevunja
kwa i, v ktk "mojo" {
kama (i == 2) {
andika("nimevunja")
vunja
}
andika(v)
}
// Tokeo:
m
o
j
nimevunjaEndelea
Tumia neno msingi endelea kuruka mzunguko maalum:
kwa i, v ktk "mojo" {
kama (i == 2) {
andika("nimeruka")
endelea
}
andika(v)
}
// Tokeo:
m
o
nimeruka
okwa i, v ktk "mojo" {
kama (i == 2) {
andika("nimeruka")
endelea
}
andika(v)
}
// Tokeo:
m
o
nimeruka
o