Kamusi Katika Nuru
Kamusi katika Nuru ni miundo ya data inayotunza jozi za funguo-thamani. Ukurasa huu unatoa maelezo kuhusu Kamusi katika Nuru, ikiwemo namna ya kutengeneza, namna ya kubadilisha, na namna ya kuzunguka ndani yake.
Kutengeneza Kamusi
Kamusi zinawekwa kwenye mabano singasinga na hujumuisha funguo na thamani zake zikitenganishwa na nukta pacha. Mfano wa uainishwaji wa kamusi:
orodha = {"jina": "Juma", "umri": 25}
orodha = {"jina": "Juma", "umri": 25}
Funguo zinawezakua tungo, namba, desimali, au buliani na thamani inaweza kua aina ya data yoyote ikiwemo tungo, namba, desimali, buliani, tupu, au kitendakazi:
k = {
"jina": "Juma",
"umri": 25,
kweli: "kweli",
"salimu": unda(x) { andika("habari", x) },
"sina thamani": tupu
}
k = {
"jina": "Juma",
"umri": 25,
kweli: "kweli",
"salimu": unda(x) { andika("habari", x) },
"sina thamani": tupu
}
Kupata Vipengele
Unaweza kupata vipengele vya kamusi kwa kutumia funguo zake:
k = {
"jina": "Juma",
"umri": 25,
kweli: "kweli",
"salimu": unda(x) { andika("habari", x) },
"sina thamani": tupu
}
andika(k[kweli]) // kweli
andika(k["salimu"]("Juma")) // habari Juma
k = {
"jina": "Juma",
"umri": 25,
kweli: "kweli",
"salimu": unda(x) { andika("habari", x) },
"sina thamani": tupu
}
andika(k[kweli]) // kweli
andika(k["salimu"]("Juma")) // habari Juma
Kuboresha Vipengele
Boresha thamani ya kipengele kwa kukipa thamani mpya kwenye funguo yake:
k = {
"jina": "Juma",
"umri": 25,
kweli: "kweli",
"salimu": unda(x) { andika("habari", x) },
"sina thamani": tupu
}
k['umri'] = 30
andika(k['umri']) // 30
k = {
"jina": "Juma",
"umri": 25,
kweli: "kweli",
"salimu": unda(x) { andika("habari", x) },
"sina thamani": tupu
}
k['umri'] = 30
andika(k['umri']) // 30
Kuongeza Vipengele Vipya
Ongeza jozi mpya ya funguo-thamani kwenye kamusi kwa kuipa thamani funguo ambayo haipo kwenye kamusi husika:
k["lugha"] = "Kiswahili"
andika(k["lugha"]) // Kiswahili
k["lugha"] = "Kiswahili"
andika(k["lugha"]) // Kiswahili
Kuunganisha Kamusi
Unganisha kamusi mbili kwa kutumia kiendeshi +
:
matunda = {"a": "apple", "b": "banana"}
mboga = {"c": "tembele", "d": "mchicha"}
vyakula = matunda + mboga
andika(vyakula) // {"a": "apple", "b": "banana", "c": "tembele", "d": "mchicha"}
matunda = {"a": "apple", "b": "banana"}
mboga = {"c": "tembele", "d": "mchicha"}
vyakula = matunda + mboga
andika(vyakula) // {"a": "apple", "b": "banana", "c": "tembele", "d": "mchicha"}
Angalia Kama Funguo Ipo Kwenye Kamusi
Tumia neno msingi ktk
kuangalia kama funguo ipo kwenye kamusi:
k = {
"jina": "Juma",
"umri": 25,
kweli: "kweli",
"salimu": unda(x) { andika("habari", x) },
"sina thamani": tupu
}
"umri" ktk k // kweli
"urefu" ktk k // sikweli
k = {
"jina": "Juma",
"umri": 25,
kweli: "kweli",
"salimu": unda(x) { andika("habari", x) },
"sina thamani": tupu
}
"umri" ktk k // kweli
"urefu" ktk k // sikweli
Kuzunguka Ndani Ya Kamusi
Zunguka ndani ya kamusi kupata funguo na thamani zake:
hobby = {"a": "kulala", "b": "kucheza mpira", "c": "kuimba"}
kwa i, v ktk hobby {
andika(i, "=>", v)
}
//Output
a => kulala
b => kucheza mpira
c => kuimba
hobby = {"a": "kulala", "b": "kucheza mpira", "c": "kuimba"}
kwa i, v ktk hobby {
andika(i, "=>", v)
}
//Output
a => kulala
b => kucheza mpira
c => kuimba
Kuzunguka ndani ya kamusi na kupata thamani peke yake:
hobby = {"a": "kulala", "b": "kucheza mpira", "c": "kuimba"}
kwa i, v ktk hobby {
andika(i, "=>", v)
}
//Output
kulala
kucheza mpira
kuimba
hobby = {"a": "kulala", "b": "kucheza mpira", "c": "kuimba"}
kwa i, v ktk hobby {
andika(i, "=>", v)
}
//Output
kulala
kucheza mpira
kuimba
Kwa ufahamu huu, unaweza ukatumia kamusi kikamilifu katika Nuru kutunza na kusimamia jozi za funguo-thamani, na kupata namna nyumbufu ya kupangilia na kupata data katika programu zako.