Tungo Katika Nuru
Tungo ni mfwatano wa herufi ambazo zinaweza kuwakilisha andiko katika Nuru. Ukurasa huu unaangazia misingi ya tungo, namna ya kuzichambua, na baadhi ya vitendakazi vilivyojengwa ndani ya Nuru kwa ajili ya tungo.
Sintaksia
Tungo zinaweza kuwekwa ndani ya alama za nukuu ""
au ''
:
andika("mambo") // mambo
fanya a = 'niaje'
andika("mambo", a) // mambo niaje
andika("mambo") // mambo
fanya a = 'niaje'
andika("mambo", a) // mambo niaje
Uunganishaji wa Tungo
Tungo zinaweza kuunganishwa kwa kutumia kiendeshaji cha +
:
fanya a = "habari" + " " + "yako"
andika(a) // habari yako
fanya b = "habari"
b += " yako"
// habari yako
fanya a = "habari" + " " + "yako"
andika(a) // habari yako
fanya b = "habari"
b += " yako"
// habari yako
Unaweza pia kurudia utungo mara kadhaa kwa kutumia kiendeshaji cha *
:
andika("mambo " * 4)
// mambo mambo mambo mambo
fanya a = "habari"
a *= 4
// habarihabarihabarihabari
andika("mambo " * 4)
// mambo mambo mambo mambo
fanya a = "habari"
a *= 4
// habarihabarihabarihabari
Kuzunguka ndani ya tungo
Unaweza kuzunguka ndani ya tungo kwa kutumia neno-msingi la kwa
:
fanya jina = "avicenna"
kwa i ktk jina {andika(i)}
fanya jina = "avicenna"
kwa i ktk jina {andika(i)}
Output
a
v
i
c
e
n
n
a
a
v
i
c
e
n
n
a
Na kwa kutumia jozi ya funguo-thamani:
kwa i, v ktk jina {
andika(i, "=>", v)
}
kwa i, v ktk jina {
andika(i, "=>", v)
}
Output
0 => a
1 => v
2 => i
3 => c
4 => e
5 => n
6 => n
7 => a
0 => a
1 => v
2 => i
3 => c
4 => e
5 => n
6 => n
7 => a
Kulinganisha Tungo
Unaweza kulinganisha tungo mbili kwa kutumia kiendeshaji cha ==
:
fanya a = "nuru"
andika(a == "nuru") // kweli
andika(a == "mambo") // sikweli
fanya a = "nuru"
andika(a == "nuru") // kweli
andika(a == "mambo") // sikweli
Vitendakazi vya Tungo
idadi()
Unaweza kupata urefu wa utungo kwa kutumia kitendakazi cha idadi()
. Haikubali vipengele vyovyote.
fanya a = "mambo"
a.idadi() // 5
fanya a = "mambo"
a.idadi() // 5
herufikubwa()
Kitendakazi hichi hubadilisha utungo kua katika herufi kubwa. Haikubali vipengele vyovyote.
fanya a = "nuru"
a.herufikubwa() // NURU
fanya a = "nuru"
a.herufikubwa() // NURU
herufindogo()
Kitendakazi hichi hubadilisha utungo kua katika herufi ndogo. Haikubali vipengele vyovyote.
fanya a = "NURU"
a.herufindogo() // nuru
fanya a = "NURU"
a.herufindogo() // nuru
gawa()
Kitendakazi cha gawa()
hugawanyisha utungo kua safu kwa kulingana na kigawanyishi fulani. Kitendakazi hichi huchukua kipengele kimoja ambacho ni thamani itakayotumika kugawanyisha utungo wako. Kama hamna kipengele chochote kitakacho wekwa, itagawanyisha utungo kwa kuangalia nafasi tupu.
Mfano wa matumizi bila kipengele:
fanya a = "lugha ya kipogramu ya nuru"
fanya b = a.gawa()
andika(b) // ["lugha", "ya", "kipogramu", "ya", "nuru"]
fanya a = "lugha ya kipogramu ya nuru"
fanya b = a.gawa()
andika(b) // ["lugha", "ya", "kipogramu", "ya", "nuru"]
Mfano wa matumizi ikiwa na kipengele:
fanya a = "Habari, salamu kutoka Dar es Salaam"
fanya b = a.gawa(",")
andika(b) // ["Habari", " salamu kutoka Dar es Salaam"]
fanya a = "Habari, salamu kutoka Dar es Salaam"
fanya b = a.gawa(",")
andika(b) // ["Habari", " salamu kutoka Dar es Salaam"]
Kwa kuelewa Tungo na namna ya kuzichambua katika Nuru, utaweza kufanya kazi vizuri na data za maandishi katika programu zako.