Maneno Tengwa
Maneno tengwa katika Nuru ni maneno yaliyohifadhiwa ambayo yana maana maalum na hayawezi kutumika kama kitambulishi cha kibadilika, kitenda kazi, au tabaka. Ukurasa huu unajadili sintaksia na matumizi ya maneno tengwa katika Nuru na vitendakazi vilivyojengwa ndani ya Nuru.
Maneno yaliyohifadhiwa
Jedwali hapa chini linaorodhesha maneno yaliyohifadhiwa katika Nuru. Maneno haya yana maana maalum katika lugha na hayawezi kutumiwa kama kitambulishi:
kweli | sikweli | unda | fanya |
kama | au | sivyo | wakati |
rudisha | vunja | endelea | tupu |
ktk | kwa | badili | ikiwa |
kawaida |
Vitendakazi Vilivyojengwa Ndani
Nuru pia inatoa vitendakazi vingi vilivyojengwa ndani ambavyo vimehifadhiwa na haviwezi kutumiwa kama vitambulishi. Vitenda kazi hivi vinatoa utendaji muhimu kwa shighuli za kawaida katika lugha:
andika | aina | jaza | fungua |
Kuelewa maneno tengwa na vitendakazi vilivyojengwa ndani ya Nuru ni muhimu sana kwa kuandika msimbo safi, fupi, na usiyo na makosa. Kwa kuheshimu maneno tengwa na maana zake maalum, unaweza kuunda programu imara zaidi na zenye uwezo wa kudumishwa kwa urahisi katika Nuru.